Mamlaka ya jeshi la
Colombia inasema idadi ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi nchini humo
imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400.
Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka
kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana .
Vikosi vya
wafanyikazi wanaoendesha shughuli za uokoaji wanasema nyingi ya barabara za
kulipotekea maporomoko hayo huko eneo la mji wa kusini mwa taifa hilo, Mocoa
hazipitiki kutokana na mkasa huo.
Maporomo hayo
yametokea baada ya mvua kali kunyesha kwa saa nyingi.
Viongozi wa mataifa
jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na
kuahidi kwenda kuisaidia Colombia.
Rais Juan Manuel
Santosa alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli
za uokoaji.
Picha zilizochapisww
kwenye mitandao na jeshi zilionyesha baadhi ya majeruhi wakiokolewa kwa kutumia
ndege.
Maporomo koya ardhi
yamekumba eneo hilo mara kadha miezi ya hivi karibuni.
Mwezi Novemba, watu 9
waliuawa kwenye mji wa El Tambo, karibu kilomita 140 kutoka Mocoa kufuatia
maporomoko ya ardhi yaliyosababiswa na mvua kubwa.
0 comments:
Post a Comment