Raia wa
Ufaransa wanapiga kura ya urais hivi leo.
Kwa mara ya kwanza baada ya miongo
kadhaa , huu umekuwa uchaguzi usiotabirika.
Takriban asilimia 30 ya wapiga kura
wanaaminika kwamba hawajatangaza msimamo wao.
Wawaniaji watatu wakuu hawana
historia yoyote ya kisiasa akiwemo Emmanuel Macron, Marine le Pen na Jean-Luc
Melenchon
![]() |
Wagombea maarufu (Kushoto kuenda kulia): François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron na Jean-Luc Mélenchon |
Mpinzani wao mhafidhina Francois
Fillon, amehudumia serikali katika nyadhfa kadhaa za uwaziri katika kipindi cha
miongo miwili.
Hakuna
yeyote anayetarajiwa kuibuka na ushindi katika duru ya kwanza, na wawili
watakaoongoza uchaguzi huo watamenyana na katika duru ya pili mwezi ujao.
Usalama umeimarishwa kufuatia shambulizi la kigaidi
lililotokea katikati mwa mji mkuu Paris alhamis, ambapo afisa mmoja wa polisi
aliuwawa.
0 comments:
Post a Comment