Saturday, 1 April 2017

AFRIKA KUSINI YAPATA WAZIRI MPYA WA FEDHA...

Waziri wa Fedha mpya wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba, amesema wakati umefika wa kubadilisha sana uchumi.

Amesema, kwa muda mrefu Afrika Kusini inahodhiwa na wawekezaji wa nchi za nje.
Pia amekiri kwamba kutolewa kazini kwa waziri aliyemtangulia hapo jana, Pravin Gordhan, kumeigawa nchi.
Bwana Gordhan anayeheshimiwa kimataifa, alipotolewa kazini ghafla, katika mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyofanya Rais Jacob Zuma, kulizuka malalamiko kutoka kwa watu wengi, pamoja na makamu wa rais, Cyril Ramaphosa, na wanasiasa mashuhuri katika chama tawala cha ANC.

Vyama vya upinzani, vinasema, Bwana Gordhan aliondolewa, kwa sababu alimzuwia Rais Zuma na washirika wake, wasipate nafasi ya kufikia mali ya taifa.

Related Posts:

  • UBUNGE WA BULAYA BADO WA NG’ANG’ANIWA… Wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maom… Read More
  • MUGABE ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 93… Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kiongozi wa taifa mwenye umri wa juu zaidi duniani kwa sasa, ametimiza miaka 93. Kiongozi huyo anatarajiwa kujumuika kwa sherehe ya faradha na jamaa, wafanyakazi wake wa karibu na baadh… Read More
  • WATU 80 MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA ARUSHA… Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limenasa watuhumiwa 80 wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, akiwemo askari Polisi mmoja mwenye namba 6978 Koplo zakayo ambaye anashikiliwa kwa mahojiano. Akizungumza leo na waandi… Read More
  • MGODI MWINGINE WAPOROMOKA MARA.. Takribani mwezi mmoja sasa tangu wachimbaji 15 wafukiwe na kifusi Nyarugusiu Wilayani Geita, balaa jingine la aina hiyo limetokea wilayani Butiama mkoani Mara, katika mgodi wa Buhemba ambapo watu 11 wameokolewa shimoni … Read More
  • MAKAMANDA WA MIKOA WATAKIWA KUONGEZA NGUVU VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA… Katika kuhakikisha kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya inakomeshwa hapa nchini na kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya, jeshi la polisi nchini limetoa maelekez… Read More

0 comments:

Post a Comment