Friday, 29 May 2015

Historia fupi ya Rais mpya wa Nigeria……


Rais mpya wa Nigeria Buhari

Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari, anaapishwa leo kama rais mpya wa nchi hiyo.

Bwana Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi anachukua uongozi kutoka kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan,ambaye amemtaka kuiunganisha nchi hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.
Buhari anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barani afrika.
Lakini je Buhari ni nani ?


 Muhammadu Buhari ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Anasemekana kuwa si m-kaishi,na hakubali kushindwa.
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,Mkristo anaye toka eneo la Niger Delta kusini Nigeria kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi.
Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?

Related Posts:

  • TIMU ZILIZOINGIA ROBO FAINALI EURO 2016.... Michuano ya Euro 2016 hatua ya 16 bora ya imemalizika tayari na hizi ndo timu ambazo zimesha ingia robo fainali baaada ya June 27 2016 kuchezwa michezo miwili ya mwisho. Mechi za robo fainali zitaanza kuchezwa June … Read More
  • UKIJAAMIANA NA UNDER 18 JELA INAKUITA..…! June 27 2016 bunge la 11 limefanya mapitio ya marekebisho ya muswada wa sheria ya mtoto, ambayo imeelekeza kuwa mtu atakayempa mimba mtoto ambaye kisheria anafahamika ni yule mwenye umri wa chini ya miaka 18, basi atahu… Read More
  • HIFADHI KUBWA ZAIDI YA GESI YAGUNDULIWA TANZANIA….!   Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi. Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu, sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi … Read More
  • PADRI APIGA MARUFUKU LIPSTICK KWA MAHARUSI….! Waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es Salaam, wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo Lipstick’ wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndo… Read More
  • SIAFU WAUA BWANA HARUSI…!! Wakazi  wa Kijiji  cha  Nditu,  Kata  ya Suma, Wilaya ya Rungwe  mkoani Mbeya, wamegoma   kuzika mwili wa marehemu Shabani  Yusufu (27),  baada kushambuliwa na kundi la … Read More

0 comments:

Post a Comment