Thursday, 28 May 2015

Marekani:Jeshi latuma Kimeta kimakosa.....

Maafisa 22 waliogusana na zana hiyo ya kimeta katika kambi ya Osnan Korea Kusini wanachunguzwa
Maafisa wakuu katika idara ya ulinzi ya Marekani wamekiri kuwa chembechembehai za ugonjwa hatari wa Kimeta zilitumwa kimakosa kwa kambi 9 za kijeshi nchini Marekani na moja nchini Korea Kusini.

Kulingana na makao makuu ya ulinzi nchini Marekani sampuli za chembechembehai za Kimeta zilidhaniwa kuwa zimekufa na hivyo zikatumwa kutumia njia ya usafirishaji mizigo ya umma kimakosa.
Chembechembe hizo za kimeta zilikuwa zimenuiwa kutumika katika mazoezi ya shambulizi la zana za kibaiolojia zakijeshi katika kambi za mazoezi.
Wandani wa maswala ya zana za kibayolojia wanasema kuwa kungetokea maafa makubwa iwapo chembechembe hizo za kimeta zingeachiliwa nje ya maabara maalum ya kibayolojia.
Maafisa wa serikali ya Marekani walioko Korea Kusini wameripoti kuwa takriban watu 22 waliogusana na zana hiyo katika kambi ya kijeshi ya Osnan wanachunguzwa.
Kimeta ni hatari ikinuswa au ikiliwa.
Hadi sasa hakuna kati yao aliyeonesha dalili za maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Wakati ukweli ulipobainika mahabara na vituo vya kijeshi vilifungwa.
Kimeta ni hatari ikinuswa au ikiliwa.
Ni silaha inayoweza kutumiwa wakati wa vita vya kemikali.

Makao makuu ya kijeshi ya Pentagon yanasema kuwa haijulikani ni watu wangapi wanaokabiliwa na hatari hiyo nchini Marekani.
Hadi uchunguzi ukamilike, hakuna bacteria zozote za kimeta zinaweza kusafirishwa kutoka Marekani.
Kambi za kijeshi zilizoathirika ni Texas, Maryland, Wisconsin, Delaware, New Jersey, Tennessee, New York, California na Virginia.
Kufikia sasa watu wanne pekee wanachunguzwa nchini Marekani


Related Posts:

  • MAHARUSI WAFUNGA NDOA KWA KUTUMIA DOLA MOJA KENYA Ushawahi kuona sherehe ya harusi isiyo na burudani wala mapochopocho na gharama husika haizidi dola moja? Basi wiki hii, Wakenya, Wilson Mutura na Ann walitumia shilingi mia moja au dola moja tu kufunga ndoa. Dola yeny… Read More
  • MANGWEA AWATOKEA CPWAA NA NOORAH.. Ikiwa sasa ni miaka minne na miezi kadhaa imepita tangu Rapa Albert Mangwea kufariki dunia, wasanii Noorah pamoja na Cpwaa kwa pamoja wamejikuta wakifanya mpango wa kuingia studio na kurudi na nguvu mpya wakidai kuwa… Read More
  • MWENYEKITI WA CCM MBEYA ANUSURIKA KUUAWA.. Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo li… Read More
  • HAKIMU MMOJA ASIKILIZA MASHAURI 400 KWA MWEZI.... Imeelezwa kuwa uhaba wa mahakimu katika Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imefanya kila hakimu katika mahakama hiyo kuwa na mzigo wa mashauri 400 kwa mwezi mmoja. kufuatia hali hiyo, mahakama imeomba Mabaraza za Ardhi ya V… Read More
  • ANASWA NA MAHINDI YA BEI CHEE KUTOKA NJE YA NCHI Mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la JAPHET amekamatwa na kikosi maalum  kinachohusisha TRA , POLISI na MAAFISA WA KILIMO akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchini Malawi bila ya kufuata u… Read More

0 comments:

Post a Comment