Wanafunzi
wa shule za msingi nchini Uganda,wamepewa mafunzo ya kijeshi kama njia ya
kupambana na kundi la ash Shabab la Somalia.
Mtandao
wa habari wa "Africa Times" umeripoti kuwa, wanafunzi wa shule za
msingi nchini Uganda wanaandaliwa kijeshi kwa ajili ya kupambana na kundi la
ash Shabab.
Kundi
la ash Shabab ambalo linaaminika kuwa na wapiganaji elfu sita huko Somalia, ni
tishio kwa Uganda.
Msemaji
wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo,amesema wanamgambo wa ash Shabab
hawawalengi wanajeshi pekee,hivyo kuna haja kwa wananchi kupewa mafunzo ya
kuweza kupambana na wanamgambo hao.
0 comments:
Post a Comment