Tuesday, 26 May 2015

Huyu mzee wa miaka 180 anatamani kufa…….!!!!



Watu wengi duniani hapa hawapendi kusikia ama kutaka kujua ni siku gani atakufa, kwa  kawaida ni kwamba kila mtu huwa anaogopa anaposikia taarifa zinazohusiana na kifo. Lakini kwa mzee Muhashta Murasi ambaye alikuwa fundi viatu aliyestaafu kazi hiyo mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka 122, amesema anakisubiri kifo kwa hamu kubwa sana kwani amechoka kuishi.
Kwa sasa ana umri wa miaka 180 na alizaliwa mwaka 1835 na tayari ameingia kwenye kitabu cha dunia cha kumbukumbu cha Guines kwa kuwa ndiye binadamuu pekee mwenye umri mkubwa kuliko wote.
Alizaliwa katika mji wa Bangalore India na kwa mujibu wa daktari aliyekuwa akimfanyia vipimo, amedhibitisha kuwa amekua hana magonjwa ya mara kwa mara hali inayochangia kuendelea kuishi kwa muda mrefu.
Lakini mtandao wa World News Report umesema huenda habari za mzee huyo hazina ukweli wowote.

Related Posts:

  • POMBE ZA VIROBA ZENYE THAMANI YA BILIONI 10.8 ZAKAMATWA DAR……. Pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki  maarufu kama ‘viroba’ zenye thamani ya shilingi Bilioni 10.8 zimekamatwa Jijini Dar es Salaam katika msako wa pombe hizo uliofanyika kuanzia Machi 01 mpaka … Read More
  • VIDEO: TIMBULO – MFUASI Timbulo ameachia video ya wimbo wake Mfuasi. Wimbo umetayarishwa kwa ushirikiano wa Maximizer & Mr. T-Touch huku video ikiongozwa na Dr. Eddie wa Dreamland Music Entertainment ya Nairobi. … Read More
  • NECTA YAZIDI KUWABANA WALIOGHUSHI VYETI Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine. Tangazo hi… Read More
  • TUNZA SIKIO KAMA YAI KWANI LIKISHAHARIBIKA NDIO BASI- WHO Zaidi ya asilimia tato ya watu wote duniani wanaishi na tatizo la kupoteza uwezo wa masikio kusikia, lakini kuzuia tatizo hilo ni rahisi kuliko kuitibu. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO katika ujumb… Read More
  • BARAKAH DA PRINCE NA NAJ KUNANI….? Barakah Da Prince alikaakitakona Mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, DJ Rodger kuzungumzia status ya uhusiano wake na Naj. Kwenye interview hiyo Barakah amedai kuwa bado mapenzi yao yapo moto moto ila wameamua kutop… Read More

0 comments:

Post a Comment