Tuesday, 26 May 2015

Utafiti:Uzito mkubwa ni hatari………

Kuwa na uzito mkubwa katika umri mdogo kunaweza kusababisha ugonjwa wa saratani ya utumbo hapo baadae.

Watafiti walikuwa wakiwafuatilia wanaume takriban 240,000, Raia wa Sweden kwa miaka 35.
Uchambuzi uliochapishwa kwenye jarida moja, unaonyesha kuwa vijana wadogo walikuwa hatarini mara mbili zaidi kupata maradhi ya Saratani ya utumbo, takwimu zilikuwa juu zaidi kwa vijana wadogo wenye uzito mkubwa .
Shirika la kimataifa la utafiti wa Saratani limesema uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani una “nguvu”.
Saratani ya utumbo ni aina ya saratani ya tatu ambayo huwakumba walio wengi duniani, ikiripotiwa kugunduliwa kwa wagonjwa milioni 1.4 kila mwaka.
Ulaji wa Nyama nyekundu na matumizi ya Mafuta kupita kiasi husababisha uzito mkubwa.
Waliojitolea kwenye utafiti huo walikuwa na umri wa kati ya miaka 16 na 20 kwa kuanzia.Wengi wao walikuwa na uzito wa kawaida,
Rachel Thomson ni mtafiti kutoka Shirika la kimataifa la utafiti wa Saratani,amesema kuwa uzito wa kupita kiasi unaweza kusababisha Kansa ya utumbo
“Matokeo haya yanaonyesha kuwa Kansa ya utumbo inaweza kusababishwa na tabia na mtindo wa maisha yetu ya kila siku” alieleza Rachel

Related Posts:

  • WATU 80 MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA ARUSHA… Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limenasa watuhumiwa 80 wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, akiwemo askari Polisi mmoja mwenye namba 6978 Koplo zakayo ambaye anashikiliwa kwa mahojiano. Akizungumza leo na waandi… Read More
  • KWA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI.. Mahakama ya Juu nchini India imefuta leseni za madaktari 634 ambao wamejipata kwenye sakata ya wanafunzi kutumia udanganyifu kujiunga na vyuo vya mafunzo ya udaktari katika jimbo la Madhya Pradesh. Mamia ya wanafunzi,… Read More
  • HIVI NDIVYO DAWA ZA KULEVYA ZINAVYOHARIBU UBONGO. Watafiti wamefanya chunguzi mbalimbali kwa kutumia wanyama kama mfano wa kazi amilifu za ubongo wa binadamu ili kufafanua michakato ya kimsingi ya dawa za kulevya katika ubongo. Mada hii ya kushangaza inashirikisha maeneo… Read More
  • VIONGOZI WA MADAKTARI KENYA WAFUNGWA JELA.. Mahakama ya masuala ya wafanyakazi nchini Kenya, imewahukumu viongozi saba wa chama cha wahudumu wa afya (KMPDU) kufungwa jela mwezi mmoja. Hatua hiyo inafuatia Viongozi hao kukaidi agizo la kumaliza mgomo ambao umedumu… Read More
  • WAFIKA POLISI KUOMBA WAPEWE DAWA ZA KULEVYA........ Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya waathirika wa dawa za kulevya maarufu kwa jina la ‘mateja’ wamefika makao makuu ya polisi mkoa wa Mbeya kuomba wapewe dawa hizo kidogo kwani zimeadimika mtaani. Waathirika hao… Read More

0 comments:

Post a Comment