Wednesday, 20 May 2015

Magari milioni 34,kurejeshwa viwandani..!!!

Mifuko ya Hewa ya Kampuni ya Takata ikiandaliwa kiwandani tayari kwa matumizi


Takriban magari milioni thelathini na nne 34,000,000 yanatarajiwa kurejeshwa viwandani nchini Marekani kufuatia hitilafu ya kiufundi kwenye mifuko ya hewa ya usalama. Kampuni inayotengeneza mifuko ya hewa ya usalama ya magari,inachukua hatua hiyo baada ya malalamiko kuwa hitilafu ya muundo wake imesababisha vifo vya watu wapatao watano.
Tukio hili la urejeshwaji wa magari viwandani kutokana na kasoro za kiufundi ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani.
Kampuni ya kutengeneza vifaa vya magari ya Japan, Takata, imekiri mifuko ya hewa kulinda usalama wa watumiaji wa magari kuwa na kasoro.
Baadhi ya mifuko hiyo ya hewa imepasuka kwa nguvu kupita kiasi,na kusababisha kurusha vipande vya chuma kwa madereva na abiria wanaokaa viti vya mbele.
Waziri wa Usafirishaji wa Marekani Anthony Foxx, ametangaza kurejeshwa kwa magari yenye hitilafu ya mfumo huo kote nchini humo.
Bwana Foxx amesema urejeshwaji wa magari hayo ni kazi kubwa.
Tangazo hilo limetolewa na Utawala wa usalama wa taifa nchini Marekani, katika barabara Kuu baada ya mazungumzo marefu na kampuni ya Takata.
Magari yanayorejeshwa yanahusu kampuni kumi na moja za kutengeneza magari zikiwemo za Honda, Toyota na Nissan.
Urejeshwaji viwandani kwa magari mapya,hufanyika baada ya kugundulika hitilafu lolote la kiufundi linaloweza kuhatarisha usalama wa watumiaji wa magari hayo.

Related Posts:

  • Kizee chauawa kwa kudaiwa mchawi,India……. Wanyama pia hutumiwa katika ushirikina Bibi kizee mmoja amenyongwa hadi kufa na wanakijiji wenzake, kwa tuhuma za ushirikina, kaskazini mashariki mwa India. Polisi katika jimbo la Assam wamesema mwanamke huyo mwenye umr… Read More
  • Mabadiliko ya muda wa kulala na saratani. Ugonjwa wa Saratani Mabadiliko katika mfumo wa kulala unaweza kusababisha mtu kupata saratani ya Maziwa. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya wanasayansi juu ya athari ya kazi za zamu kiafya. Utafiti unaonesha kuwa wanawak… Read More
  • New Joint from Mambo band-Dadavua Wanafahamika kama Mambo Band,kundi linaloundwa na vijana watatu P.Man Star,Yuyu na Musa Bhai,wenye maskani yao mitaa ya Sekei-Kaza moyo Arusha. Ngoma yao inafahamika kama DADAVUA imefanyika katika studio zao wenyewe zinazo… Read More
  • Matumaini ya tiba ya ubongo…….! Maradhi ya Alzheimer huua seli za ubongo Data zinasubiriwa kwa hamu kuhusu dawa inayotumainiwa kuponya ugonjwa wa udhoofu wa ubongo (Alzheimer) baadae leo. Watafiti watatangaza matokeo ya uchunguzi kuhusu matumizi ya … Read More
  • Kitimtim michuano ya Klabu Bingwa Ulaya... Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya inaendelea tena hii leo kwa timu zile zinacheza round yakwanza ambapo Dila Gori ya Geogia itakuwa na kibarua kigumu itakapoumana vikali na Partizan Belgrade ya Serbia. Huku FC Pyunik ya Arm… Read More

0 comments:

Post a Comment