Monday, 11 May 2015

Kanisa labadilishwa kuwa msikiti Itali..!!!!

Iceland imezua hisia kali wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya usanii katika mji wa Venice nchini Italy baada ya kulibadilisha kanisa ambalo lilikuwa halitumiki kuwa msikiti.

Kwa jina 'La Moschea' msikiti huo unatokana na jengo la santa Maria della Misericordia,kanisa moja la kikatholiki ambalo lilikodishwa na Iceland na mwenyewe.
Na ili kuonyesha uvumilivu wa kidini waislamu wengi walijitokeza kuomba katika jumba hilo kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Wakiwa wamewacha viatu nje ya lango la jumba hilo,waumini hao walielekea Mecca na kusujudu huku wageni wakiendelea na ziara zao za za utalii katika jumba hilo.
Uwekaji wa msikiti huo ulifanywa na msanii mmoja wa Switzerland Christoph Buechel kwa lengo la kuvutia hisia kutokana na kutokuwepo kwa hata msikiti mmoja katika mji wa kihistoria wa Venice--mji ulio na uhusiano wa kihistoria na ulimwengu wa kiislamu.
Lakini mamlaka ya mji huo imeonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo ikisema kuwa jengo hilo lina hatari ya kushambuliwa na wale wanaopinga Uislamu ama Waislamu wenye itikadi kali.
Rais wa jimbo la Veneto Luca Zaia ametaja hatua hiyo kama uchochezi.

Related Posts:

  • Dewji apata tuzo ya uongozi... Mtanzania mfanyabiashara maarufu na Rais wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (MO) ,ameibuka mshindi wa tuzo ya Mtu aliyefanya vizuri katika Uongozi kwa Mwaka 2016 inayotolewa na Jarida la African Leadership. Dewji am… Read More
  • MAJAJI WAJINOA MAHAKAMA YA UFISADI…!! Jaji Mkuu wa tanzania Mohamed Chande amesema kuwa, jopo la majaji linatarajiwa kuingia darasani ili kujifunza sheria mpya ya kuendesha kesi za ufisadi.  Kesi hizo zitakuwa zinaendeshwa katika Mahakama Kuu Kite… Read More
  • Watu 3 huhitaji viungo bandia kila siku MOI. TAASISI ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), imesema katika idadi yote ya majeruhi wanaowapokea, kila watu 50 wanaofika kunakuwepo na moja ambaye anakuwa ameumia zaidi mguu ama mkono ambao mwishowe inabidi uondolewe. Changa… Read More
  • Jammeh asema ataondoka madarakani.... ..... Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa. Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya hata tone moja la damu kumw… Read More
  • OBAMA AMALIZA MUDA WAKE IKULU YA WHITE HOUSE.. Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa na mkutano wake wa mwisho na waandishi habari Ikulu mjini washington, tukio la mwisho la shughuli zake rasmi , kabla ya kumkabidhi madaraka Rais mteule Donald Trump. Obama aligusia … Read More

0 comments:

Post a Comment