Wednesday, 20 May 2015

Je wewe ni mnunuzi wa bidhaa za urembo. ?

Tahadhari.
Kinyesi cha panya na mkojo wa binadamu ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeza bidhaa ghushi za urembo.

Utafiti wa bidhaa za urembo zinazouzwa kwa njia ya mtandao nchini Uingereza umebaini kuwa bidhaa hizo zina tengezwa kwa njia isiyofata maadili na kulinda afya ya binadamu.
Utafitri huo uliochunguza bidhaa za urembo kama vile vipodozi marashi na mafuta ya kujipaka iligundua kuwa zinaongezwa madini ya sumu kama vile arsenic.
Kwa mujibu wa Polisi waliotekeleza uchunguzi huo, mfumuko wa bei ya bidhaa kwa njia za kielektroniki kumechangia pakubwa ongezeko la mauzo ya bidhaa gushi.
''ni vigumu sana kubaini uhalali wa bidhaa haswa unaponunua kwa njia ya kielektroniki kwa sababu unachokiona hapo mtandaoni ni picha tu ya bidhaa halali''
''sasa bidhaa hiyo inapokufikia huwa tayari umekwisha lipia na ni vigumu sana kwako kurejesha bidhaa hizo pindi unapokuwa hujaridhia ubora wake'' alisema afisa aliyesimamia uchunguzi huo.
Marashi mengi yanamkojo wa binadamu na sumu ya arsenic

Bidhaa za kielektroniki zinazopendelewa na wafanyibiashara walaghai ni kama zile zile zinazosokota nywele na pia zingine zinazotumika kwa ususi.
Hata hivyo bidhaa hizo haziwezi kuhimili matumizi ya muda mrefu na hivyo zinahatarisha maisha ya watumizi kutokana na hatari kulipuka.
Isitoshe Polisi wanasema kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa marashi ghushi yanayouzwa London yanajumuisha sumu aina ya Cyanide na mkojo wa binadamu.
Vipodozi vimepatikana na sumu aina ya arsenic madini yenye sumu ya zebaki na risasi .
Vipodozi hivyo vinaweza kusababisha kujikuna,vipele visivyokwisha na maradhi mengine ya ngozi.
Bi Maria Woodall, anayeongoza kitengo cha uchunguzi wa hati miliki ya bidhaa alionya kuwa watu wengi hawafahamu madhara ya kutumia bidhaa ghushi.

Related Posts:

  • HII NDIO NOTI YENYE MWONEKANO MZURI DUNIANI…!! Mkutano wa Mwaka wa ‘International Bank Note Society’s ‘IBNS’, umetambua ubunifu wa kutengeneza noti za fedha zenye muonekano mzuri na usalama zaidi. Katika mkutano wao wa mwaka IBNS wameitan… Read More
  • ASHINDA TUZO AKIWA MAHABUSU…..!! Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC), umempa tuzo ya mwaka George Mgoba aliye mahabusu akikabiliwa na shtaka la kuandaa kinyume cha sheria maandamano ya vijana, waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga T… Read More
  • MTOTO WA MIAKA 2 AMUUA MAMAKE KWA BUNDUKI..!! Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa, katika mji wa Milwaukee nchini Marekani. Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari. Mwanamke huyo Patrice Price 26 alikuwa akie… Read More
  • ALIYEVUMBUA PLEASE CALL ME ASHINDA KESI…!! Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini, imeiamuru kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kumlipa mwanamume aliyebuni wazo la kutuma ujumbe wa kuomba apigiwe simu. Gazeti la Sowetan la Afrika Kusini linasema kuwa mwajiri… Read More
  • WATU KUFANYA KAZI SIKU MBILI KWA WIKI VENEZUELA…!! Serikali ya Venezuela imeagiza wafanyakazi wake wawe wakifanya kazi siku mbili kwa wiki,hii ni hatua ya muda iliyochukuliwa kutokana na uhaba wa umeme. Makamu wa Rais Aristobulo Isturiz ametangaza kwamba, watumishi wa… Read More

0 comments:

Post a Comment