Aliyekuwa
Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais
kupitia tiketi ya Chadema.
Mwanasheria wa Chadema, Tundu
Lissu amesema baada ya kuchukua fomu hizo Lowassa atakuwa tayari kuzunguka nchi
nzima kujitambulisha kwa wananchi kama mgombea rasmi wa Chadema.
Lissu amesema uamuzi wa
kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda
usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais
chini ya chama hicho.
Amesema katiba ya Tanzania
inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule
aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo
Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba
Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais.
0 comments:
Post a Comment