Monday 3 August 2015

Yupo msichana wa miaka 15 tu anasoma PhD …

Kwa hesabu ya kawaida tu mtoto anaanza Shule ya msingi akiwa na miaka sita au saba hivi,alafu mpaka kumaliza anakuwa na kama miaka 14, sasa kuna msicha  kwenye umri huo alikuwa kamaliza high school na alikuwa Chuo tayari anamaliza zake degree!!

Anaitwa Sushma Verma ni msichana ambaye umri wake ni miaka 15, aligraduate Degree ya Microbiology Chuo cha Lucknow kilichopo India na kajiunga Babasaheb Bhimrao Ambedkar University (BBAU) kwa ajili ya kusomea Masters, kamaliza mwezi June 2015 na anaendelea kujipanga ili kuendelea na masomo ya PhD.

Sushma amewashangaza wengi lakini ndio hivyo, ana uwezo mkubwa sana darasani kitu ambacho Mkuu wa Chuo hicho amemuahidi kumpa ofa ya kulipiwa ada pamoja na Hostel bure akianza PhD ya environmental microbiology.

0 comments:

Post a Comment