Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, amewataka wakazi wa
jijini hilo kuchukua hadhari za kiafya ikiwamo kuacha kusalimiana kwa kushikana
mikono kutokana na mlipuko wa kipindupindu ambao mpaka sasa umeshawapata watu
56, kati yao watatu wamefariki dunia.
Akizungumza jana ofisini kwake mbali
na kushikana mikono, Sadik amewataka wananchi kuacha kunywa maji ya viroba
maarufu kama “maji ya Kandoro” na juisi za mitaani ili kupunguza uwezekano wa
kupata ugonjwa huo.
Amesema ugonjwa huo ulilipuka Agosti
15 baada ya mtu mmoja kufariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala.
Amesema idadi ya wagonjwa
imeongezeka hadi kufikia 56, lakini mpaka sasa wamebaki wagonjwa 36 katika
kituo maalumu kilichofunguliwa Mbagala baada ya wengine kutibiwa na kuruhusiwa
kurudi nyumbani.
0 comments:
Post a Comment