Wanasayansi nchini Marekani wamesema
kuwa, wamefanikiwa kutengeneza chachu yenye vina saba vinavyoweza kupunguza
maumivu kwa kiasi kikubwa.
Chachu
hiyo inaweza kubadilisha sukari kuwa hydrocodone, dawa inayofanana na morphine
ndani ya siku tatu mpaka tano.
Kwa sasa inachukua takribani
mwaka mzima,kuzalisha kundi la dawa za kutuliza maumivu kama hayo, kutoka
kwenye mmea aina ya popi.
Hata
hivyo watafiti kutoka chuo cha Stanford wamesema kuwa, kazi zaidi inahitajika
kwa sababu utafiti wao umeegemea zaidi kwenye matumizi ya chachu nyingi, kutengeneza
kidonge kimoja pekee cha kutuliza maumivu
0 comments:
Post a Comment