Utafiti mmoja uliofanywa nchini
China,umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea
maisha marefu.
Utafiti huo haswa umeonesha kuwa
ukila chakula hususan pilipili, utaishi maisha marefu zaidi duniani.
Watafiti mjini Baijing walidadisi
maisha na vyakula wanavyokula wenyeji, nusu milioni katika kipindi cha utafiti
cha miaka 7.
Utafiti huo ulibaini kuwa wale
waliokula chakula kilichojumuisha pilipili, walikuwa katika hali bora zaidi
kiafya wala hawakuwa katika hatari ya kuaga dunia.
Hali yao ya siha ilitofautiana
sana ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini ya
siku moja kwa juma.
Watafiti hao walitoa tahadhari.
Wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa
wa ushahidi tu, lakini wakashauri utafiti zaidi ufanyike kwengineko ilikutilia uhakika
utafiti wao.
Hata hivyo walibaini kwa uhakika
kuwa kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana
na seli zinazotuma ujumbe kwa ubongo, kuwa mtu amezeeka na kusababisha
viashiria vya utu uzima.
0 comments:
Post a Comment