Kampuni
iliyodaiwa kutengeneza simu bandia elfu 41 aina ya Iphones kutoka kampuni ya
Apple, imevamiwa huko Uchina na watu 9 kukamatwa.
Oparesheni hiyo ilishirikisha
mamia ya wafanyikazi waliokuwa wakiandaa vipuri vya simu, vilivyotumika kama
simu mpya aina ya iphone tayari kuuzwa nje, huku simu hizo bandia zikizalisha
kitita cha dola miloni 19.
Kampuni hiyo iligunduliwa tarehe
14 mwezi Mei, lakini ikabainika katika mitandao ya kijamii na ofisi ya usalama
ya umma Beijing siku ya jummapili.
Oparesheni hiyo ilianzishwa mwezi
wa januari,na uchunguzi huo uliongozwa na kundi la mke na mumewe kaskazini mwa
mji mkuu wa Uchina, kulingana na mamlaka ya Beijing.
Wamesema kuwa walidokezewa na mamlaka ya Marekani ambayo
ilinasa simu hizo bandia .
Ripoti hiyo inajiri wakati kuna
msako wa bidhaa bandia unaotekelezwa na Uchina, huku mamlaka hiyo ikiyashinikiza
makampuni kuweka nembo za ubora wa biadha.
Uchina pia imekubali kufanya kazi
na mamlaka ya Marekani, kupunguza kuwepo kwa bidhaa bandia zinazotoka nchi hizo
mbili.
0 comments:
Post a Comment