Wednesday 5 August 2015

Ripoti ya TFDA kuhusu vipodozi vilivyoteketezwa 2014/15…

Mmlaka ya chakula na Dawa TFDA, imeatoa ripoti ya mwaka wa fedha kuhusu bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na kuteketezwa kwa mujibu wa sheria na hatua zilizochukuliwa.


Mkurugenzi wa TFDA Hitti Sillo amesema katika mwaka wa fedha wamekamata na kuteketeza vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku tani 16.61 ambazo thamani yake ni shilingi milioni 44.2.

Amesema kazi hiyo ni endelevu kwa kuwa TFDA ipo sehemu mbalimbali nchini, na wakaguzi wake wapo kuanzia bandarini na katika viwanja vya ndege ambapo ndipo hukamataa bidhaa nyingi.

Amesema miaka mitatu iliyopita udhibiti umeimarika sana, ndio maana matukio mengi ya kukamatwa kwa watu ambao wanaingiza vipodozi hatari kinyume cha sheria wanakamatwa wakiwa mipakani.

0 comments:

Post a Comment