Thursday 20 August 2015

Kufanya kazi kwa saa nyingi ni hatari……

Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya watu laki tano, umeeleza kuwa watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi, wako hatarini kupata kiharusi.

Takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu la Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida.
Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi, wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu.
Wataalamu wanasema kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida, na kukaa kwa muda mrefu ni mbaya kwa afya na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi.

Daktari Kivimaki ameuambia Mtandao wa Habari wa BBC kuwa,watu wanapaswa kuwa makini na afya zao, kuangalia mtindo wao wa maisha na kuhakikisha wanapima vipimo vya damu kuepuka shinikizo la damu.

0 comments:

Post a Comment