Wafanyakazi wa shirika la umeme nchini Madagascar
wamegoma kazi kulalamikia hali mbaya ya kimaisha.
Mgomo huo ambao umekuja baada ya ule wa
wafanyakazi wa shirika la ndege nchini humo, ulianza jana Jumatatu ambapo
wafanyakazi hao walilalamikia mshahara wa chini wanaolipwa na serikali.
Migogoro ya kijamii na migomo ya kila mara katika
sekta tofauti za serikali, ni changamono nyingine ambayo imewasukuma wabunge
kuzidisha mashinikizo kwa serikali ya Rais Hery Rajaonarimampianina, ambapo
hivi karibuni bunge la nchi hiyo lilipitisha kwa wingi wa kura muswada wa
kutokuwa na imani na rais huyo, kwa madai ya kukiuka katiba na kutokuwa na
uwezo wa kuongoza nchi.
Hii ni katika hali ambayo tayari walimu wa shule
za msingi na wale wa vyuo vikuu na kadhalika wafanyakazi wa taasisi za kitaifa
nchini Madagascar, wametangaza kuanza mgomo wao siku chache zijazo.
Mgomo wa mwezi mmoja wa wafanyakazi wa shirika la
ndege ambao ulifanyika kuanzia tarehe 17 Juni mwaka huu, ulipelekeakuvunjwa
safari za ndege na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi hususan katika sekta
ya utalii.
Weledi wa mambo wanatabiri kuwa, kuendelea migomo
hiyo, kunaweza kumfanya Rais Hery Rajaonarimampianina kujiuzulu.
0 comments:
Post a Comment