Mahakama
moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela, kwa
kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi.
Katika kikao hicho Mahakama kuu
ya Kenya mjini Kisumu, imempata na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka
25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limebanwa.
Hakimu mwandamizi Aswani Opande
alimpata na hatia bwana Okewo, kwa kumabaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo
cha miaka 100 jela.
Katika shtaka la pili hakimu huyo
mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni, alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka
mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa
Ukimwi.
Hakimu alimpata na hatia bwana
Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe.
Upande wa mashtaka unasema kuwa
bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi,
kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.
![]() |
Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia''
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9
anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio
hilo.
|
Alipopewa fursa ajitetee, mshtakiwa
aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo.
Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa
kumuonea huruma, na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake
na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake,hata hivyo amepewa siku 14 kukata
rufaa.
0 comments:
Post a Comment