Monday 17 August 2015

Kitabu cha kuchuja maji chagunduliwa…

Kitabu chenye kurasa ambazo zinaweza kuraruliwa na kisha kutumiwa kuchuja maji ya kunywa, kimepata mafanikio katika majaribio yake ya kwanza.

Kitabu hicho pia kina maandishi ya ujumbe kuhusu jinsi maji yanaweza kuchujwa.
Kurasa za kitabu hicho zina kemikali maalum, ambayo huua viini vilivyo kwenye maji wakati maji yanapochujwa kwa kutumia kurasa zake.
Majaribio 25 yameshafanyika kwenye maji machafu katika nchi za Afrika kusini, Ghana na Bangladesh, karatasi kutoka kwa kitabu hicho zilifanikiwa kuondoa asilimia 99 ya viini kutoka katika maji hayo.
Ubora wa maji ulipatikana baada ya kuchujwa kwa maji machafu, ulifikia viwango vya ubora wa maji ya mfereji nchini Marekani
Dr Teri Dankovich ambaye ni mtafiti katika chuo cha Carnegie Mellon mjini Pittsburg, aliunda na kujaribu teknolojia ya kitabu hicho kwa miaka mingi.
Teknolojia hiyo itatumiwa na jamii kwenye nchi zinazoendelea,na pia dunia nzima ukizingatia kuwa watu milioni 663 kote duniani hawapati maji safi ya kunywa.
Anasema kuwa kile mtu anachotakiwa kufanya ni kurarua kitabu na kuweka karatasi, na kuitumia kuchuja maji ambayo hutiririka yakiwa masafi na yasiyo na viini.
Dr Dankovich tayari ameifanyia majaribio katarasi hiyo katika mahabara akitumia maji yaliyochafuka.

Baadaye aliifanyia majaribio akitumia maji machafu ambayo yamechafuka kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita ambapo ilipata mafanikio makubwa.

0 comments:

Post a Comment