Wizara ya afya nchini kenya imetoa orodha ya peremende, keki na biskuti, bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi.
Katika kile ambacho kinatarajiwa
kuwashanga wazazi, barua ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba mahabara ya serikali,
ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu, keki
na mandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.
![]() |
Peremende zenye bangi zauzwa Kenya |
Licha ya watoto kuvipenda bidhaa hizo, serikali inataka
vipiwe marufuku na kuondolewa kabisa madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kiziuza.
Kupitia kwa barua kwenda kwa
wakuu wa afya wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya imewaamrisha
maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu zingine bidha hizo
zinaweza kupatikana.
0 comments:
Post a Comment