Watu wengi
wanawachukia, lakini mbu sasa husherekewa kwa tamasha la kipekee katika mji
mmoja huko nchini Urusi.
Pengine la ajabu zaidi kwenye hafla hiyo ni kuwepo kwa
mashindano ya kuchagua msichana mrembo zaidi, ambapo wasichana hao watahukumiwa
kulingana na idadi ya alama za kuumwa na mbu baada ya kusimama kwa muda wa
dakika 20 wakiwa wamevalia suruali fupi na fulana ndogo.
Jopo la majaji
wataalamu wakiwepo madaktari wataikagua miili yao na mshindi atakua yule
atakaye kuwa na alama nyingi za kuumwa na mbu, asema mratibu wa sherehe hiyo
Natalya Paramonova.
Mwaka 2013, mshindi alikuwa na alama hizo za kuumwa na mbu mara
100.
Kwa wale wanao shangazwa na wazo hilo la kujitolea kuumwa na
mbu hao, kuna mengine, shughuli ndogo ndogo zengine za ajabu zimezinduliwa
ikiwepo shindano la kuona ni nani anayeweza kushika mbu aliye hai.
0 comments:
Post a Comment