Mwanamme mzee
zaidi duniani raia wa Japan Sakari Momoi, ameaga dunia mjini Tokyo akiwa na
umri wa miaka 112.
Mwalimu huyo mkuu wa zamani wa shule ya upili na baba wa
watoto watano, aliaga dunia kutoka na ugonjwa wa figo katika kituo kimoja cha
kuwahudumia watu wazee siku ya Jumapili.
Alikuwa ametambuliwa na Guinness World Records mwezi Agosti.
Momoi alizaliwa mwaka 1903 mjini Fukushima na alikuwa mwalimu
kabla ya kupanda cheo na kuwa mwalimu mkuu kwenye shule kadha nyumbani kwao.
Wakati alipopata cheti kutoka kwa Guinness World Records
mwezi Agosti, aliwaambia waandishi wa habari alitaka kuishi miaka miwili zaidi.
Guinness bado
haijatangaza mwanamamme mwenye umri mkubwa zaidi duniani baada ya Momoi.
Mtu ambaye aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na
Guinness ni Jeanne Calment kutoka ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku
164.Aliaga dunia mwezi Agosti mwaka 1997.
0 comments:
Post a Comment