Wabunge
wa Rwanda wamepiga kura jana Jumanne kuunga mkono mabadiliko ya katiba, ili
kumruhusu rais Paul Kagame awanie muhula wa tatu madarakani, wakiunga mkono
waraka ulotiwa saini na mamilioni ya raia.
Bunge zima lililojaa wananchi waliokwenda
kushuhudia utaratibu mzima, lilisherehekea na kuimba jina la Kagame baada ya
wabunge wote waliokuwepo katika mabaraza yote mawili ya bunge kupiga kura
katika hatua ya kwanza ya utaratibu kwa ajili ya mabadiliko ya katiba.
Spika wa bunge Donatillla
Mukabalisa, amesema kwa maneno yake “ninataka kuwashukuru wabunge wote kwa
kuonyesha uungaji mkono matarajio ya wananchi”.
Zaidi ya
watu milioni 3.7 ambao ni zaidi ya nusu ya wapiga kura walitia saini nakala ya
kutoa wito kwa mabadiliko ya kipengele namba 101 cha katiba, ambacho
kinamdhibiti rais kuhudumu kwa miaka miwili, kwa mujibu wa vyombo vya habari
vya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment