Thursday, 9 July 2015

Udukuzi wa Marekani dhidi ya Ujerumani……

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa,nakala za siri zilizochapishwa katika mtandao wa wikileaks hapo jana,zinanonesha kuwa shirika la usalama wa taifa la Marekani limekuwa likiwafanyia udukuzi machansela wa tatu waliotangulia wa nchi hiyo.

Nakala hizo zimeonesha kuwa Marekani waliweka vifaa vya kurekodi kisiri katika simu za wasaidizi wa Chansela Merkel wa Ujerumani na watangulizi wake watatu, akiwemo Gerhard Schroeder na Helmut Kohl.
Mwaka mmoja uliopita Ujerumani ilimuagiza afisa mkuu wa intelijensia wa Marekani jijini Berlin aondoke mara moja kufuatia madai hayo kuwa walikuwa wakimfanyia udukuzi Angela Merkel.
Hata hivyo mwezi uliopita waendesha mashtaka wa Ujerumani walilazimika kusitisha uchunguzi wao wakisema kuwa shirika hilo la Marekani la NSA imekataa kutoa ushahidi waliotaka.

0 comments:

Post a Comment