Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kiongozi wa taifa
mwenye umri wa juu zaidi duniani kwa sasa, ametimiza miaka 93.
Kiongozi huyo
anatarajiwa kujumuika kwa sherehe ya faradha na jamaa, wafanyakazi wake wa
karibu na baadhi ya maafisa wakuu serikali.
Sherehe kubwa rasmi,
inayotarajiwa kugharimu zaidi ya dola milioni moja za Kimarekani, itaandaliwa
siku ya Jumamosi.
Rais Mugabe aliongoza
Zimbabwe kupata uhuru wake mwaka 1980 na ametangaza kwamba anapanga kuwania
katika uchaguzi mkuu mwaka ujao, ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.
Mugabe alizaliwa 21
Februari, 1924.
Alifungwa jela
1964-1974 kwa kutoa "hotuba ya kuhujumu serikali"
Baada ya kuachiliwa,
alisaidia kuongoza vita dhidi ya serikali ya Rhodesia
Vita vilipomalizika,
Mugabe alishinda uchaguzi 1980 na akawa waziri mkuu wa Zimbabwe na akaongoza
taifa hilo kama waziri mkuu hadi mwaka 1987.
Anaposherehekea
kutimiza miaka 93, Umoja wa Ulaya umepiga kura kuongeza vikwazo dhidi yake.
Vikwazo hizo vinahusu
usafiri, kuzuiliwa kwa mali yake na kupiga marufuku biashara ya silaha baina ya
mataifa wanachama wa EU na Rais Mugabe, mkewe na wizara ya ulinzi ya Zimbabwe.
Hata hivyo, baraza la EU lilipiga kura kuondoa sehemu ya
marufuku ya ununuzi wa silaha dhidi ya Zimbabwe.
Umoja huo sasa utaruhusu taifa
hilo kuagiza kutoka nje vilipuzi ambavyo vinatumiwa katika uchimbaji wa madini
na ujenzi wa miundo mbinu.
Vikwazo hivyo vitatathminiwa upya
mwaka ujao.
EU ilimuwekea Mugabe vikwazo mara
ya kwanza mwaka 2002 baada ya kuvamiwa kwa mashamba yaliyomilikiwa na Wazungu
pamoja na tuhuma za wizi wa kura uchaguzini na ghasia na dhuluma dhidi ya
upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu.
Rais Mugabe anasema vikwazo hivyo
vimesababisha madhila yasiyo na kifani kwa nchi yake, na kwamba ni sehemu ya
mpango wa Uingereza kutaka kumuondoa madarakani.
0 comments:
Post a Comment