Mbunge wa Hai Freeman Aikaely Mbowe,
mfanyabiashara mkubwa nchini, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima
wametajwa kwenye orodha ya pili ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
ya watu mashuhuri wanaohusishwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya.
Makonda amemtaja pia mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azan na
mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali kwenye orodha hiyo.
Ameielezea orodha
hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana
taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara
hiyo.
Watu hao
watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya
kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.
Wengine wanaohitajika ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club,Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.
0 comments:
Post a Comment