Tuesday, 21 February 2017

WANAWAKE WAPIGWA MARUFUKU KUSAFIRI PEKE YAO LIBYA…

Maafisa wa kijeshi wanaodhibiti eneo la mashariki mwa Libya, wametangaza marufuku kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 60 ya kuwazuia kusafiri nje ya nchi wakiwa peke yao.

Marufuku hiyo inatajwa kutokana na sababu za kiusalama wa taifa na wala si kwa misingi ya kidini.
Mwandishi wa BBC wa Kaskazini mwa Afrika, anasema kuwa marufuku hiyo, itaathiri abiria wote wanaopita eneo la mashariki mwa nchi.
Libya imegawanyika pande mbili moja mashariki na serikali inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake mjini Tripoli.
Serikali ya mashariki ina makao yake mjini al-Beyda, na marufuku hiyo ilianza kutekelezwa kwanza katika uwanja wa ndege wa mji huo wa Labraq.
Msemaji wa mkuu wa majeshi mashariki mwa Libya Abdulrazzak al-Naduri alithibitisha hatua hiyo kwa BBC.
Wakati wa mahojiano ya runinga, alidai kuwa wanawake wanaowakilisha makundi ya kijamii ambao husafiti mara kwa mara nje ya nchi hutumiwa na mashirika ya kijasusi ya kigeni.

Marufuku hiyo haijapigiwa kura na bunge lakini tayari imenaza kutekelezwa mashariki mwa nchi.

0 comments:

Post a Comment