Thursday, 2 February 2017

MUME AMKATA MKE WAKE MASIKIO…

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zarina mkazi wa mji wa Balkh Afghanistan, amekatwa masikio na mume wake kwa madai kuwa mume wake amemchoka na hataki kuishi nae.

Akielezea tukio hilo la kikatili Zarina alisema amedumu na mwanaume huyo kwa muda wa miaka saba na tukio hilo lilitokea wakati akiwa amelala usiku lakini ghafla aliamka na kukuta akifanyiwa tukio hilo.
“Sikuwa nimemfanyia jambo lolote baya, sijui kwanini mme wangu alinifanyia hivi … mahusiano yetu hayakuwa mazuri,” alisema Zarina.
Mwanamke huyo mwenye miaka 21 aliongeza kuwa mume wake amekuwa akimfanyia vitendo vya kikatili kwani kuna kipindi alimzuia hata kwenda kuwatembelea wazazi wake.
Aidha Zarina alizungumza kuhusu mpango wake wa baadae kama ataendelea kuishi na mwanaume huyo na kusema, “Sihitaji tena kuishi nae.”

Zarina kwasasa anapatiwa matibabu katika moja ya hospitali iliyopo Balkh na Polisi mjini humo wamesema mume wake amekimbia na juhudi za kumtafuta zinafanyika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment