Katika Kuadhimisha Siku ya
Saratani duniani, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Asasi ya Marafiki wa Watoto
wenye Saratani Tanzania (FoCC) Janeth Manoni, amesema kwa sasa ugonjwa huo
umekuwa tishio kwa watoto nchini, ambapo inakadiriwa zaidi ya watoto 25,000
hupata ugonjwa huo kila mwaka.
Manoni ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa watoto wengi hufariki dunia baada
ya kuchelewa kupata matibabu kufuatia jamii kutojua dalili za awali za
ugonjwa huo..
Manoni amesema asasi yake
itaadhimisha siku ya saratani Jumamosi ya Februari 18 katika viwanja vya Don Bosco,
ambapo kutatolewa huduma za uchunguzi wa saratani kwa watoto bure, na kuwataka
wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kufanyiwa uchunguzi.
Mhamasishaji wa FoCC Remigius Kazaura amesema kuwa, ongezeko la ugonjwa
wa saratani kwa watoto linatokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha hasa ulaji
wa vyakula visivyo vya asili.
0 comments:
Post a Comment