Sunday, 5 February 2017

Rais wa Ukrain afanya mazungumzo ya simu na Trump

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko, amesema kuwa amekuwa na mazungumzo na Donald Trump, kuhusiana na hali ilivyo mashariki mwa nchi hiyo, mahali ambapo majeshi ya serikali yanakabiliana na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Bwana Poroshenko, amesema kwamba, Bwana Trump, amezungumzia kuimarisha mikakati ya ushirikiano kati ya Ukraine na Marekani, na haja ya kutanzua mgogoro huo kwa njia ya kidiplomasia.
Mapigano mapya mashariki mwa Ukrain
Urusi kuvuruga matangazo ya radio kutoka Ukrain kwenda Crimea
Awali, Bwana Poroshenko alisema kuwa, mapigano mapya yaliyochipuko huko hivi majuzi, inaimarisha haja ya Marekani kuiwekea vikwazo Urusi.
Lakini Bwana Trump amesema kuwa, anataka kuimarisha uhusiano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment