Mama mmoja mkazi wa Tanga, Sabaha Ally mjane mwenye watoto wawili amejitokeza mbele ya Rais Magufuli akiwa ameshika bango lenye maelezo na kutaka msaada kutoka kwa Rais.

Mama huyo aliyejitokeza mbele ya Rais kueleza kero ya masuala ya mirathi alifanyaa maamuzi hayo leo Februari 2, 2017 wakati Rais Magufuli akimaliza kuhutubia yake katika maadhimisho ya siku ya Sheria yaliyofanyika viwanja vya Mahakama Ocean Road.