Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji
akiwa na umri wa miaka 84.
Tshisekedi alikwenda mjini Brussels
mwishoni mwa mwezi january kwa ajili ya matibabu.
Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa
wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.
Alisimama kidete katika utawala wa
aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake
ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.
Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani
wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae
Rais Joseph Kabila ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment