Bunge limepitisha kwa kauli moja,
azimio la kuitwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti ili kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na
Madaraka ya Bunge.
Azimio
hilo limetokana na hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara
akisema wateule hao wa Rais wametoa kauli zinazodhalilisha hadhi ya mhimili huo
wa Dola.
Akijibu
swali kuhusu tuhuma dhidi yake zilizoibuliwa na wabunge kuhusu chanzo cha mali
zake, Makonda amewaambia waandishi wa habari kuwa wakati mwingine watunga
sheria hao hulala bungeni kwa kukosa cha kuzungumza.
Aidha,
kutokana na wabunge kukerwa na kauli ya Makonda, mbunge wa Mkuranga (CCM),
Abdallah Ulega ameomba mwongozo kuhusu suala hilo.
Hata
hivyo, Mkuu wa wilaya, Mnyeti anadaiwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook
kuwa wabunge ni wapuuzi kutokana na michango yao wakati walipohoji hatua ya
Ma-DC na Ma-RC kutoa amri za kuwaweka mahabusu viongozi wa kisiasa
0 comments:
Post a Comment