Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK
umefungiwa.
Uamuzi huo umekuja saa
chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA Jumatano
hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu
dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza
kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na
hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram. “Napokea simu
nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji
taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu
ya jambo hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza
popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na
siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili
usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa
#SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.”
Mbunge
wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook: Serikali
imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni utani kumbe
Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”
USIKILIZE WIMBO HUO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment