Muhandisi wa zamani wa shirika la maswala ya angani Nasa ameajiriwa na
kampuni ya teksi Uber kusaidia katika utafiti wake wa kutengeza magari
yanayoruka.
Mark Moore
anajiunga na Uber kama mkurugenzi wa uhandisi wa angani.
Lengo la Uber
katika kutengeza magari yanayoruka liliangaziwa mwezi Oktoba ambapo maswala ya
kupaa na kutua yalijadiliwa.
Uber tayari
inawekeza katika magari ya kujiendesha ikishirikiana na kampuni ya Volvo na
Daimler.
Katika mipango
yake Uber imesema kuwa katika mahitaji ya angani ,kampuni hiyo ina uwezo wa
kuimarisha uchukuzi wa mijini na kuwapatia wateja wake muda wanaopoteza kila
siku wanaposafiri.
''Huku majumba marefu yakisaidia katika
utumizi mchache wa ardhi, uchukuzi wa mijini utatumia maneeo matatu ya angani
kukabiliana na msongamano wa magari ardhini''.
Mpango huo
utashirikisha mtandao wa ndege za kielektroniki ambazo zitapaa na kushuka wima.
Moore alifichua
mpango kama huo katika jarida lililochapishwa wakati alipokuwa Nasa.
Alisema kuwa
mpango wa kutengeza vitu vinavyopaa kielektroniki ni mpango muhimu wa
kiteknolojia wa ndege na kuongezea kwamba kitu kinachozuia kuanza kwa mpango
huo ni betri zitakazotumika.
Kampuni ya
kutengeza magari ya ya Aeromobil kutoka nchini Slovakia ni miongoni mwa kampuni
ambazo zina mpango wa kutengeza gari la kuruka ambayo inatarajiwa kuingia
katika soko mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment