Mahakama ya masuala ya wafanyakazi nchini Kenya, imewahukumu viongozi
saba wa chama cha wahudumu wa afya (KMPDU) kufungwa jela mwezi mmoja.
Jaji Hellen Wasilwa amesema
viongozi hao hawajatoa sababu ya kutosha kuonesha ni kwa nini hawajamaliza
mgomo huo.
Ameamuru mazungumzo ya kumaliza mgomo huo yaendelee.
Jaji Wasilwa alikuwa awali
amewapa viongozi hao muda wa wiki mbili kumaliza mgomo huo, na baadaye
akawaongezea siku tano.
Mazungumzo ya kumaliza mgomo
huo hata hivyo hayakuzaa matunda kipindi hicho.
Madaktari wamekuwa wakiitaka
serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013, ya kuwaongezea mishahara.
Wamekataa mshahara
walioongezewa na serikali wa asilimia 40 wakisema kuwa ni wa chini kuliko ule
walioafikiana mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment