Tuesday, 14 February 2017

PLAYBOY KUCHAPISHA TENA PICHA ZA UTUPU..

Jarida la Playboy limetangaza kwamba litaanza kuchapisha tena picha za utupu, na kubatilisha uamuzi wa awali uliotolewa mwishoni mwa mwaka jana.

Hatua ya sasa imetangazwa na afisa mkuu mpya wa ubunifu katika jarida hilo Cooper Hefner, ambaye amesema uamuzi wa kuondoa kabisa picha za utupu "lilikuwa kosa".
"Leo tunarejesha utambulisho wetu na kutwaa tena sifa zetu," aliandika kwenye Twitter.
Jarida hilo linalochapishiwa Marekani pia limepakia mtandaoni jalada la makala yake ya Machi-Aprili ya jarida hilo na kutumia kitambulisha mada #NakedIsNormal (Utupu ni kawaida).
Baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wamefurahia uamuzi huo, lakini wengine wamesema uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu majarida hayo hayanunuliwi sana.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment