Chama kinachotawala
nchini Zimbawe Zanu-PF, kimeanza kuchangisha pesa kwa sherehe za siku ya
kuzaliwa ya Rais Robert Mugabe ambaye anahitimiza miaka 93.
Waandalizi wa sherehe
hizo wanasema kuwa wanataka kuchangisha ng'ombe 150 kwa chakula.
Gazeti la serikali la
Herald limemnukuu mbunge Never Khanye, akisema kuwa hakuna mtu atalazimishwa
kuchanga lakini wakulima wakubwa katika maeneo ya matabeleland ambapo shehere
zitafanyika, ni lazima watoe ngombe mmoja kila mmoja, kutoa asante kiongozi
huyo wa miaka mingi.
Wakulima wakubwa ni
wale walipata mashamba makubwa kutoka kwa serikali kufuata hatua ya serikali ya
kunyakua mashamba kutoka wa wazungu wakati wa programu iliyokumbwa na utata
nchini Zimbabwe.
Chama cha Zanu-PF
kinasema kuwa kinatarajia karibu watu 100,000 kuhudhuria sherehe hizo.
Shere hizo zitafanyika
eneo la Matobos nje kidogo ya mji wa Bulawayo.
0 comments:
Post a Comment