Wednesday 1 February 2017

MVUA YALETA MAAFA WILAYANI MPWAPWA…

Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja ambao ni wakazi wa Kijiji cha Isighu kitongoji cha Majumba Sita wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wamekufa maji baada ya makazi yao kusombwa na mvua iliyo nyesha usiku wa kuamkia Januari 31.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wilaya ya Mpwapwa Dkt. Said Mawji amekiri kupokea miili ya watu wanne na majeruhi wawili.
Aidha, amewataja waliofariki kuwa ni Maritha Mabula, Shukuru Donald, Bernadeta Mabula na mwingine ni Jeska Lubeleje.
Amesema majeruhi wawili waliojeruhiwa kwenye mafuriko hayo ni Beka Mlami na Joseph Sumisumi ambao teyari wametibiwa na kuondoka.
Mzee wa familia hiyo, Mabula Sumisumi, amesema hakuwepo katika mji huo siku hiyo alienda kulinda mifugo kambini ndipo alipoambiwa familia yake imesombwa na maji.

Hata hivyo, Sumisumi alisema kila kitu kilichokuwamo ndani kimesombwa na maji ikiwamo akiba ya chakula na fedha kiasi alizokuwa amehifadhi ndani ya nyumba ambazo hakuzitaja kiasi chake.

0 comments:

Post a Comment