Monday 30 January 2017

AHUKUMIWA KIFUNGO KWA KULALA NA MPENZI WA MWANAE…

Mwanamke mmoja ambaye ametambulika kwa jina la Alaine Goodman (46) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na kijana mwenye umri mdogo ambaye ni mpenzi wa mtoto wake.

Goodmann alipandishwa kizimbani katika mahakama ya New York, Marekani ambapo alisomewa shitaka la kufanya mapenzi na kijana wa miaka 13 jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi hiyo.
Mwanamke huyo anadaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari na kijana huyo ambaye ni mpenzi wa mtoto wake wa kumzaa, kitendo ambacho kilifanyika Machi 15, 2015.
Wakili wa Goodmann, James Liguor alimwambia jaji wa mahakama hiyo kuwa ampunguzie kifungo kwani hata yeye anajutia kitendo hicho, “anaumizwa na jambo hilo, linamuuma kama jinsi wengine linavyowauma.”

Katika upelelezi ambao ulifanyika awali ulionyesha kuwa mwanamke huyo baada ya kufaya mapenzi na kijana huyo alimtumia ujumbe kwenye simu wa kumsifia na hata walipolichunguza gari walilolitumia zilikutwa alama ambazo zilionyesha wazi kuwa kuna watu wamefanya mapenzi ndani ya gari.

0 comments:

Post a Comment