Maelfu ya waandamanaji walikusanyika Jumapili karibu na White House huko Washington DC kwa siku ya pili ya malalamiko katika miji mikubwa kote Marekani dhidi ya marufuku ya safari iliyotolewa na Rais Donald Trump kutoka nchi saba za kiislam.
Waandamanaji
wakipiga kelele “Hakuna chuki, Hakuna Khofu, Wakimbizi wanakaribishwa hapa,
waandamanaji waliishambulia amri ya Rais Trump ambayo inawazuia wakimbizi wote
kuingia Marekani angalau kwa siku 120.
Amri hiyo
pia inazuia viza kutoka raia wa Somalia, Sudan, Libya, Yemen, Iran na Irak kwa
siku 90 na marufuku kama hiyo kwa raia wa Syria. Malalamiko yanafanyika hasa
katika miji ya New York, Los Angeles, Philadelphia, Houston, Boston, Atlanta,
Louisville na Detroit.
Watu kadhaa walishikiliwa kwa muda
wa siku nzima Jumapili walipowasili Marekani kutoka baadhi ya nchi hizo na
kuachiwa huru baada ya mahakama kuingilia kati.
0 comments:
Post a Comment