Jeshi la
Marekani limesema askari wake mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika
shambulizi lake lililokuwa limeelekezwa kwa kikundi cha al-Qaida huko Yemen.
"Tumesikitishwa
sana na kifo cha askari wetu katika kikosi maalumu cha 'Elite'," amesema
kamanda wa Kikosi cha Central Command cha Marekani," Jenerali Joseph
Votel.
"Kujitolea
huku ni kwa hali ya juu katika vita yetu dhidi ya magaidi ambao wanahatarisha
maisha ya watu wasio na hatia ulimwenguni."
Taarifa
iliyotolewa na ofisi ya Central Command ya Marekani imesema wapiganaji 14 wa
Yemen wenye mafungamano na kundi la al-Qaida waliuwawa katika mashambulizi
haya.
Ndege
ya kivita ya jeshi la Marekani ilioshiriki katika shambulizi hilo ilishindwa
kuendelea na zoezi hilo kwa sababu ya kushindwa kutua na kusababisha matatizo
zaidi kwa askari wake, taarifa hiyo imesema ndege hiyo iliangamizwa.
Viongozi
wa makabila na vyanzo vya habari vya Yemen vimedai kuwa viongozi wa ngazi ya
juu wa al-Qaida walikuwa kati ya wale waliouwawa.
Mashambulizi
hayo yalifanyika katika jimbo la Bayda.
0 comments:
Post a Comment