Jengo la Amani na Usalama lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, limetangazwa rasmi kuwa litaitwa Mwalimu Julius Nyerere.
Jengo hilo limepewa
jina hilo rasmi katika hafla iliyofanyika jana na kuhudhuriwa na Rais Dkt. John
Magufuli pamoja na marais mbalimbali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika,
Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Antonio Guterres, mawaziri na mabalozi mbalimbali wanaohudhuria
Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika unaoendelea nchini
Ethiopia.
Kwa mujibu wa taarifa
ya Ikulu, Rais Magufuli amewashukuru viongozi wote wa AU kwa kuamua jengo hilo
liitwe jina la Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutambua mchango wake katika
kupigania amani na usalama na amebainisha kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mwafrika
halisi na kiongozi mahiri na shupavu.
0 comments:
Post a Comment