Saturday, 21 January 2017

NYAMA KUANZA KUTENGENEZWA MAABARA..

DUNIA inabadilika kwa haraka kutokana na maendeleo katika sekta mbalimbali. Teknalojia nayo inakua kwa kasi huku ikitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu.

Siku hizi Dunia inashuhudia uvumbuzi wa teknalojia za kisasa katika nyanja za kilimo, afya, nishati na nyingine nyingi.
Kila kukicha wanasayansi wanafanya jitihada za kutengeneza nyama katika maabara.
Tunafahamu kuwa aina zote za vyakula vinavyotumiwa na binadamu inatokana na mimea na wanyama.
Mamilioni ya wanyama huchinjwa kila siku duniani kwa ajili ya kupata kitoweo.
Uchinjaji wa wanyama umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji jambo ambalo limewafanya wanasayansi kufikiri namna ya kutengeneza kitoweo hiki muhimu pasipo kuhusisha kuchinja mnyama.
Rasilimali nyingi zimekuwa zikitumika kulisha wanyama, kuwachinja na kusafirisha, pia kumekuwapo upotevu mkubwa wa maji na nishati katika mzunguko mzima wa kupata kitoweo hiki.
Ufugaji wa wanyama ambao hutupatia nyama unazalisha gesi ya methane ambayo inamchangio mkubwa katika mabadiliko ya tabianchi, wanasayansi wanataka kuondokana na haya yote kwa kutafuta mbinu mbadala ya kuzalisha nyama.
Kwa upande mwingine, wanyama hufungiwa ndani kwa maisha yao yote. Wanyama pia huchinjwa kikatili ili kuweza kupata nyama. Pamoja na haya yote, ni vigumu kufikiri maisha ya binadamu bila kula nyama.
Utamaduni wa kula nyama ni mkongwe duniani na kwa vyovyote vile haitakuwa rahisi kuufuta.
Kwa kutambua ukweli huu, wanasayansi wameaanza kutengeneza nyama maabara waliyoipa jina la nyama ya Vitro au Vitro meat kwa kimombo.
Nyama ya Vitro huzalishwa maabara. Kwa kawaida nyama hutengenezwa kutokana na kemikali ndogo inayojulikana kitaalamu atoms.
Kama unaweza kutengeneza atoms kwa njia tofauti na ya kawaida, basi pia unaweza kutengeneza nyama.
Ukipewa vipande viwili vya nyama kimoja kilichotokana na mnyama aliyechinjwa na nyingine aina ya Vitro ambayo hutengenezwa maabara ni vigumu kuelezea tofauti yake kutokana na kufanana kwa muonekano na hata ladha.
Maabara sasa inafanya kazi ya kutengeneza nyama ambayo ni sawa na nyama uliyozoea kununua buchani. Profesa wa Molecular Biology, katika Chuo Kikuu cha Stanford, alinukuliwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza akisema inawezekana kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama kwa kuwa nyama sasa inaweza kutengenezwa maabara.
Gharama kubwa za uzalishaji wa nyama ya Vitro inaweza kuwa ndiyo kikwazo kikubwa katika uzalishaji wake. Hata hivyo, ugunduzi zaidi kwenye teknalojia ya uzalishaji wake itaweza kupunguza gharama.
Kampuni kubwa ikiwamo New Harvest na Modern Meadow zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nyama hii inazalishwa kwa wingi na kuwafikia walaji wengi.

0 comments:

Post a Comment