Rais wa Ufilipino
Rodrigo Duterte amesema Marekani inahatarisha usalama wa eneo kwa kuendelea
kurundika silaha zake katika nchi hiyo.
Rais Duterte ameituhumu
Washington kuwa inatengeneza vituo vya kudumu vya kuhifadhi silaha zake katika
mikoa mitatu ya nchi hiyo. Rais wa Ufilipino amesema: "Ninatoa ilani kwa
vikosi vya jeshi la Marekani, sitoruhusu muendelee kuhifadhi silaha zenu katika
ardhi yetu, hata hatufahamu kama makombora ya nyuklia yanaingizwa nchini na US
au la."
Amebainisha kuwa, hatua hiyo ya Marekani ya kuingiza mashehena
ya silaha nchini humo inakiuka moja kwa moja makubaliano ya ushirikiano wa
kiulinzi kati ya nchi mbili hizo.
Oktoba mwaka jana, Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino
alitangaza kuwa anataka ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo vikosi vya
jeshi la Marekani viwe vimekwisha ondoka katika ardhi ya nchi yake; na kama
italazimu anataka pia kuvunja mkataba wa ulinzi na muitifaki huyo wa muda mrefu
wa Manila.
0 comments:
Post a Comment