Monday, 30 January 2017

MWENYEKITI WA CCM MBEYA ANUSURIKA KUUAWA..

Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni  kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi.
Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri.

Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea

Related Posts:

  • TANZANIA KINARA WA SOKO LA SIMU AFRIKA… Ripoti ya mwaka 2016 ya Uchumi wa Simu za Mikononi Afrika inasema kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi nane Afrika zenye soko kubwa la simu za mikononi. Ripoti hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana kwenye mk… Read More
  • MAELFU WAANDAMANA KUMPINGA RAIS BRAZIL… Polisi katika mji wa Sao Paulo Brazil, wametumia vitoa machozi kuyatawanya maandamano makubwa zaidi ya kupinga Rais mpya Michel Temer. Maandamano zaidi dhidi ya kiongozi huyo yalifanyika katika mji wa Rio de Janeiro.Wa… Read More
  • PANYA SASA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO…! Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), kimepata suluhisho la kupunguza kuzaliana panya nchini kwa kuanzisha uzazi wa mpango kwa wanyama hao. Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa Kilimo w… Read More
  • LIL WAYNE ASTAAFU MUZIKI… Lil Wayne ametangaza kwamba amestaafu kutoka kwenye tasnia ya muziki. Aliandika kwenye Twitter: "Sasa sijiwezi tena, haka kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu." Hata hivyo, hajafafanua iwapo ataa… Read More
  • 2016 WAELEKEA KUWA MWAKA WENYE JOTO KALI KUWAHI KUREKODIWA..! Mwaka huu wa 2016 huenda ukawa ndio wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa, kufuatia hali ya joto duniani kuweka rekodi mpya ya viwango vya nyuzi joto katika miezi sita ya kwanza. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Hali y… Read More

0 comments:

Post a Comment