Abiria waliokuwa
wakisafiri kwa ndege aina ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL) kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam, walipata hofu baada ya ndege yao
kuruka na muda mfupi baadae kulazimika kutua tena katika Uwanja wa Ndege wa
Mwanza
Tukio hilo lilitokea
jana saa 2.20 asubuhi uwanjani hapo, baada ya ndege hiyo kuruka kisha ikatua
ndani ya dakika 20
Wakati ndege hiyo
ikitua, Rubani aliwataarifu abiria kuwa wanalazimika kurejea uwanjani hapo
kutokana na dharura iliyojitokeza
Aidha, baadhi ya
watumishi wa uwanja huo wamesema walishangazwa kuona ndege hiyo ikirejea muda
mfupi baada ya kuruka, hali ambayo hutokea pindi ndege inapokuwa na hitilafu ya
kiufundi
“Unajua ndege nyingi
huanguka wakati wa kuruka na kutua, ndiyo maana jambo hili lilitisha abiria
hata wafanyakazi,lakini hakukuwa hitilafu kubwa ya hatari kwani baada ya
kurejea na kukaguliwa, ilionekana mlango wa mizigo ya ndege hiyo haukufungwa
vizuri, hivyo kuwasha taa ya tahadhari na Rubani kuamua kutua kwa
dharura”amesema mmoja wa watumishi hao.
Akielezea tukio hilo,
mmoja wa abiria waliokuwa uwanjani hapo aliyekuwa akitarajitarajia kusafiri na
ndege nyingine, amesema kuwa wakati ndege hiyo inatua kwa dharura, wafanyakazi
wa uwanja huo walionekana kuwa bize kiasi cha kuwashtua wasafiri waliokuwepo
uwanjani hapo.
Kwa upande wake Meneja
wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza Easter Madale, amekiri kuwapo kwa tukio hilo la
mlango ingawa amesema hakujua sababu zake.
“Tukio hilo lipo,
lakini siwezi kulizungumzia kwa sababu linawahusu watu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege,Kwa hivyo nakuomba uwatafute hao kwasababu ndio wanaojua, ingawa
linaonekana halikuwa tatizo kubwa kwani baada ya kutua, ilikaa muda mfupi na
kuondoka tena”, amesema Madale.
0 comments:
Post a Comment